Tuesday, May 17, 2016

Jinsi ya kutumia namba mbili za whatsapp kwenye simu moja

Whatsapp ni moja ya mtandao wa kijamii ambao una watumiaji wengi ambao kwa mujibu wa play store iinaonyesha kuwa Whatsapp imekuwa downloaded zaidi ya 1 billion. Whatsapp imekuwa moja ya njia inayotumiwa na watu wengi kuwasiliana pamoja na kutumiana picha,video na document.


Kumekuwa na kiu na wimbi kubwa la wadau wa Blog hii wakiniuliza kama wanaweza kutumia namba mbili za whatsapp kwenye simu moja.Kutokana na hali hiyo basi kama kawaida yangu nitawaonyesha hatua kwa hatua ili nanyi muweze kutumia multiple accounts kwenye simu zenu.

Hatua #1
Ingia kwenye play store kisha Download app inaitwa Parallel Space kisha install


Hatua #2
Fungua app yako ya Parallel Space ambayo automatic itakuwa imekuja icon ya facebook na instagram kama ambavyo inaonekana katika picha ya hapo chini
                                                                            

Hatua #3
Bonyenza kitufe chenye alama + kisha ongeza app yako ya whatsapp ama pamoja na app nyingine zozote  uzipendazo
 
Hatua #4 
Jisajili kwa namba yako mpya na ufurahie ulimwengu wako mpya wa technologia kisha usisahau ku share na wenzako nao wafurahie maujanja kutoka Mandasi Technologies Blog
 
 
LIKE our Page for daily UPDATES
Mandasi Technologies

1 comment:

  1. Positive site, where did u come up with the information on this posting?I have read a few of the articles on your website now, and I really like your style. Thanks a million and please keep up the effective work.
    Wedding Anniversary Appreciation Messages for Wife Funny

    ReplyDelete